Meli (Jahazi) ya "Omar Mukhtar" imesafiri leo kutoka bandari ya Tripoli, Mji Mkuu wa Libya, kujiunga na Kikosi cha Mshikamano wa Kimataifa na kusaidia watu wa Gaza.
Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la AhlulBayt (a.s) -ABNA- Meli ya "Omar Mukhtar" leo imeanza safari yake kutoka bandari ya Tripoli, mji mkuu wa Libya, kwa lengo la kujiunga na msafara wa kimataifa wa “Usimame Imara” (صمود) na kuonyesha mshikamano na watu wa Gaza. Kabla ya kuondoka kwa meli hiyo, kulifanyika mkusanyiko wa kuonyesha uungwaji mkono kwa Gaza mbele ya bandari hiyo.
Omar Al-Hassi, Waziri Mkuu wa zamani wa Libya ambaye pia yupo kwenye safari hii, alisema:“Lengo letu ni kuvunja mzingiro uliowekwa dhidi ya Ukanda wa Gaza. Msafara huu hauwakilishi serikali yoyote, chama chochote, wala kundi lolote - bali ni kitendo cha kibinadamu tu cha kufikisha misaada kwa watu walioko chini ya mzingiro.”
Kwa mujibu wa al-Hassi, Meli hiyo ya Omar Mokhtar imebeba wanaharakati 15 kutoka mataifa mbalimbali yakiwemo Uingereza, Canada na Scotland, huku waliosalia wakiwa ni Walibya.
Meli hiyo imebeba misaada ya kibinadamu ikijumuisha:
1-Dawa
2-Chakula
3-Nguo za watoto
4-Vifaa vya kitabibu.
Riyadh Al-Saqi, mmoja wa waandaaji wa msafara kutoka Libya, alitangaza kuwa safari hii ya ishara inatarajiwa kufika Gaza ndani ya siku 7 hadi 10. Alieleza kuwa lengo kuu ni kuondoa mzingiro dhidi ya watu wa Gaza na kuitikisa dhamira ya dunia ili iondokane na aibu ya ukimya na kutowajibika kimaadili.
Your Comment